
Serikali ya Tanzania leo imesaini mikataba miwilini na serikali ya Denmark ikiwa ni sehemu ya kudumisha mahusiano ya nchi hizi mbili katika baadhi ya maeneo yakiwemo ya uchumi na kijamii.Mikataba hiyo imesainiwa mbele ya rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Kikwete na waziri Mkuu wa Denimark Helle Thorning ambaye yupo nchini kwa siku tatu kuanzia jana kwa mwaliko rasmi wa kiongozi huyo wa Tanzania.
Mkataba wa kwanza unazungumzia makubaliano ya kuwasafirisha kwa uangalizi maalumu watuhumiwa wa uharamia wanaokamatwa katika bahari ya hindi ambao umesainiwa na waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Benard membe kwa niaba ya Tanzania na balozi wa Denimark nchini Johhn Frento kwa niaba ya nchi yake.
Katika mkataba wa pili ambao umesainiwa na waziri wa fedha Dk. Wiliam Mgimwa kwa niaba ya Tanzania na balozi Frento unazungumzia makubaliano ya kuyaendeleza mahusiano mazuri ya chuo cha wadenishi kilichopo jijini Arusha.
Akiongea mbele ya wandishi wa habari Ikulu jijini Dar es salaam mara baada ya kutiliana sahini mikataba hiyo, Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Kikwete amepongeza mahusiano mazuri yaliyopo baina ya nchi hizi mbili na kuelezea baadhi ya manufaa ambayo Tanzania itayapata kutokana na makubaliano hayo.
Kwa upande wake Waziri Thorning amesema mbali na makubaliano yaliyofikiwa hii leo, nchi yake itaendelea kusaidia Tanzania katika kupambana na umasikini hasa kwa kuwekeza katika elimu hasa kwa wanawake. source ebony fm iringa
No comments:
Post a Comment