
Venezuela imetangaza siku 7 za maombolezo baada ya kifo cha rais wa muda mrefu wa nchi hiyo, Hugo Chavez kilichotokana na maradhi ya saratani.Kifo cha Chavez aliyekuwa na umri wa miaka 58 kilichotokea jana kimesababisha huzuni tele katika taifa hilo ambalo kwa sasa litalazimika kufanya uchaguzi mkuu wa mapema kwa mujibu wa katiba ya taifa hilo utafanyika baada ya siku 30.
Makamu wa rais wa nchi hiyo, Nicolas Marduro aliyetangaza kifo hicho amesema serikali imeliamrisha jeshi na vikosi vingine vya usalama pamoja na polisi kuwalinda raia pamoja na kuhakikisha amani katika kipindi hiki kigumu.Wananchi wa Venezuela bado wamegawika baada ya uchaguzi uliofanyika mwezi Oktoba mwaka jana.
Makamu huyo wa rais aliyeteuliwa na rais Hugo Chavez ndiye anayebakia kukaimu madaraka kama kiongozi wa mpito hadi uchaguzi huo utakapofanyika...source ebonyfm.com
No comments:
Post a Comment