Wednesday, March 6, 2013

Matokeo ya awali katika uchaguzi wa Kenya yaonesha mchuano mkali kwa wagombea wawili wa nafasi ya Urais

 uhuru kenyata
Matokeo ya awali ya kura zilizohesabiwa katika uchaguzi wa Kenya bado yanaendelea kutolewa ambapo mchuano mkali kati ya wagombea wawili wa Urais Uhuru Kenyata na Raila Odinga ukishuhudiwa.
Matokeo hayo yanaonesha tofauti ya kura 589,847 na mgombea urais kupitia muungano wa kisiasa wa Jubilee, Uhuru Kenyatta anaongoza kwa kura milioni 2,792,025 sawa na asilimia 53.36 dhidi ya mpinzani wake Raila Odinga wa muungano wa kisiasa wa CORD, aliyepata kura milioni 2,202,178 sawa na asilimia 42.06
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya-IEBC, Isaack Hassan, amesisitiza kuwa matokeo rasmi ya uchaguzi huo yatatangazwa rasmi baada ya siku sita zijazo huku zaidi ya kura 309,416 zikiwa zimeharibika.
Mshindi katika uchaguzi huo, anatakiwa kupata zaidi ya asilimia 50 ya kura, vinginevyo wagombea wawili wa juu watalazimika kuingia katika awamu ya pili ya uchaguzi mwezi Aprili, mwaka huu....source ebonyfm.com

No comments: