
Hata hivyo mama wa mtoto huyo hakuhudhuria mazishi hayo kutokana na majeraha makubwa aliyoyapata pindi alipojaribu kuwadhibiti wateka nyara kumpoka mtoto wake.
Tangu wakati huo mama huyo amelazwa katika hospitali ya rufaa bugando alikofanyiwa upasuaji wa kichwa.
Shughuli hiyo ya mazishi imefanyika wakati miito zaidi ikiongezeka kukabiliana na vitendo vya kushambuliwa raia wenye ulemavu wa ngozi ambavyo vimegharimu maisha ya zaidi ya raia 70 wenye ulemavu huo.
Hapo juzi mkuu wa umoja wa mataifa nchini Tanzania Alvaro Rodriguez alitaka kuchukuliwa hatua za dharura kudhibiti vitendo hivyo.
Picha:
Tunaomba radhi kwa ukakasi wa picha, lakini huo ndio mwili wa kichanga Yohana Bahati ulivyokutwa baada ya polisi kugundua.
chanzo ni page ya redio ebony fm Iringa katika ukurasa wa facebook
No comments:
Post a Comment