Friday, February 20, 2015

Tanzania haiko tena kwenye kundi la nchi 10 maskini zaidi duniani, kwa mujibu wa Ripoti ya hivi karibuni kabisa ya Benki ya Dunia.

Kulingana na Benki ya Dunia, ripoti hiyo mpya imezingatia masuala kama pato la taifa, linalojumuisha jumla ya thamani ya bidhaa zilizozalishwa kwa kipindi fulani, mara nyingi kwa mwaka, lililogawanywa kwa idadi ya watu ndani ya nchi husika.

Kufuatia ripoti hiyo Tanzania sasa inaondoka kwenye kundi la aibu ingawa haijawa wazi iwapo mwenendo wa kutembeza bakuli kusaka msaada kutoka nchi tajri duniani litafikia kikomo.
Wakati huo huo ripoti hiyo inakuja huku hali ya kipato cha mtanzania mmoja mmoja ikisalia duni na gharama za maisha zikiendelea kupanda.

No comments: