Thursday, February 19, 2015

Wavuvi kwenye bwawa la Mtera wameitisha kikao jioni hii

Wavuvi kwenye bwawa la Mtera wameitisha kikao jioni hii kujadili mwenendo wa kushambuliwa kila mara na vikobo wa bwawa hilo katika kikao kitakachozingatia pia kumshutumu Afisa Uvuvi wa Wilaya ya Iringa kwa kutochukua hatua.

Afisa uvuvi wa wilaya ya hiyo Raphael Fuvagwa anashutumiwa kwa kupuuzilia mbali malalamiko ya wakazi hao licha ya taarifa za mara kumfikia.


Kikao hicho kinafuatia kushambuliwa kwa Mkaazi Luka Kinyaga na mnyama boko Luka Kinyaga siku ya jumatatu akiwa mhanga wa 16 kwa mwaka huu pekee na viboko wanaokutikana kwa wingi kwenye bwawa hilo.

Wakati huo huo kikao hicho kinaketi muda mfupi baada ya wavuvi na wafanyakazi wa shirika la Umeme Tanesco eneo la Mtera kuopoa sehemu ya mwili wa Salmin Malingumu mkazi wa mtera aliyeshambuliwa na kuuwawa na mamba hapo jana.

No comments: