Rapper aliyepotea kwenye ramani ya muziki wa Tanzania,
Kalapina, yupo kwenye hatua za mwisho za kuanza kushoot filamu yake
itakayozungumzia tukio la kutekwa na kupigwa kwa Dr. Steven Ulimboka.
Akizungumza na 255 ya XXL, Clouds FM, Kalapina amedai kuwa
kinachomkwamisha kwa sasa ni bajeti ya filamu hiyo.
Hata hivyo amesema amepewa ahadi ya shilingi milioni 3 kutoka
Profesa Ibrahim Lipumba kusaidia kukamilisha maandalizi yake.
Amewataka wadau wengine wamuunge mkono kwakuwa anataka
kuwaonesha watanzania utofauti katika filamu za Tanzania.
Amesema filamu nyingi za hapa nchini zimejikita katika visa
vya kufikirika na mapenzi na yeye anakuja na filamu inayozungumzia tukio la
kweli (based on a true story)
Ameongeza kuwa script ya filamu hiyo ipo tayari na wahusika
wote katika filamu wameshapatikana.
No comments:
Post a Comment