Msanii wa hiphop Kalapina wa
kikosi cha Mizinga amekubali kutaja majina ya wasanii wa hiphop
anaosikiliza muziki wao kwa sasa hapa Tanzania.
Namkariri akisema “Tanzania
mimi nasikiliza wasanii wote niangalie vitu wanavyovifanya lakini
wasanii wengi hawako real wanafake, sasa hivi nimekua nikiwasikiliza
wadogo zangu Lunduno, Nash Mc, Fid Q, Mansu Lee, Rado… mzee mwenzangu
Profesa J amepotea sasa hivi, nilikua namsikiliza lakini sasa hivi
amepotea”
“Profesa J amefikia hatua
anafanya video za dada zetu wako uchi kabisa na ule ni udhalilishaji wa
kijinsia kama atabisha si udhalilishaji, achukue video awachukue dada
zake na mama zake wadogo awavalishe vichupi na sidiria tutaona kweli
yeye ni mmagharibi lakini kama anachukua dada za watu huu ni
udhalilishaji wa kijinsia mi napinga mambo kama yale, tusifikie huko
sasa hivi huwezi kufanya video kali mpaka uweke wanawake wako uchi
Tanzania” – Kalapina
Kalapina alipoulizwa kama
ameshawahi kuongea na Profesa J kuhusu hilo amejibu “Prof sijabahatika
kukutana nae kwa karibu lakini najua ujumbe huu utamfikia kwa sababu
yeye ni mtu mzima na haya maneno ni mazito na sio kwa uadui, kwa ajili
ya kujenga Profesa jina kubwa kabisa ni mtu ambae ana hadhi kubwa kwenye
game hii hapa lakini namkumbusha, binadamu sometimes tunajikwaa
tunapotea, namkumbusha kwa kweli sijapendezwa na video zile madada wako
uchi kabisa chupi na sidiria, ule ni udhalilishaji wa kijinsia alafu
hawa wanaharakati wa kutetea haki za wanawake siwasikii kupigia kelele
maswala haya”
Kwenye line nyingine Kalapina
amesema “nyimbo zangu zote nimekua nikizungumza haki za binadamu natetea
wanyonge na ndio maana nimekua naonekana mtu tofauti na watu wengine
sipewi ile support ya kutosha leo
hii Wafalme wa hiphop wanaitwa akina Roma, hawa ni vijana wadogo zangu
sana tungo zao kama unataka kuzilinganisha na zangu ni sawa sawa
mwanafunzi wa nusery school umlinganishe na mwanafunzi wa chuo kikuu”
No comments:
Post a Comment