Roy ni producer mwenye kipajikutoka studio za G2 Records, alijishughulisha na nyimbo kali ya Vailet ya Mtonya na nyinginezo zaidi.
Hata hivyo alikua na kipaji cha kupiga kinanda(PIANO). Ambapo mnamo mwaka 1985 akiwa nchini Uingereza alishiriki mashindano ya kupiga chombo aina ya piano na kuibuka mshindi na kujinyakulia tuzo iliotambulika kwa jina la SEVEN OAKS THREE ARTIST FESTIVAL.
Pamoja na ujuzi wa muziki Roy pia alikuwa mtaalamu wa mambo ya Kompyuta, Graphics.
jamaa kabla ya kifo chake alikua akisumbuliwa na maradhi ya ini na ni ugonjwa ambao ulimpelekea kwenda kutibiwa nyumbani kwao mbeya alijiuguza takriban miezi mitatu ndipo alipo kutwa na umauti wengi waliuzunishwa sana na kifo chake akiwemo mtangazaji wa kituo cha radio cha ebony fm kilichopo mkoani iringa anaitwa edwin bashir nilifanya nae intervew kipindi nipo radio mwangaza fm dodoma jamaa alielezea hisia zake pia nakumbuka niliongea na matonya coz kati ya wasanii ambao roy aliwatoa kimuziki kwa kuwatengenezea truck nzuri na zikaheat sana ukiachilia na mr brue pia katokea kwenye mgongo wa roy wakiwemo wasanii wengi na kitu ambacho roy alikua hakipendi ilikua ni dharau jamaa dharau hakuipenda kabisa na baadhi ya wasanii waliokua wanakwenda studio wakiwa wanaonesha dharau jamaa aliwapotezea haikujalisha kama msanii alikua na jina kiasi gani ,,,,,,, Roy alikua akifanya kazi studio za G-record kwa kipindi kirefu na baada ya kukorofishana na meneja au mmiliki wa studio zili Guru ramadhani aka G-rover aliamua kujichanga na kufungua studio yake aliipa jina la G2 mpaka mauti yalipo mkuta.
Kwa kweli tumepata pigo kubwa sana, Roy tutakukumbuka daima.
No comments:
Post a Comment