Thursday, November 8, 2012

BABY MADAHA AJIUNGA RASMI NA KUNDI LA TMK WANAUME HALISI







Baby Madaha ambaye ni zao la Bongo Star Search ambaye ameshafanya poa kwenye muziki na pia upande wa filamu hapa nchini.Singer huyu wa “Amore” na “Nimezama” baada ya kuchonga na BK Cop aliweza kufunguka na kusema kuwa kwa sasa amejiunga rasmi na kundi la TMK Wanaume Halisi linaliundwa na member kama Juma Nature, Dollo, KR na wengine wengi.
Kuhusu sababu zilizompelekea kufanya kazi na TMK Wanaume Halisi, Baby Madaha alifunguka na kusema kuwa kundi ilo ni kundi la wasanii ambao wanafanya kazi na si wale ambao wanakuwa na majungu kwenye kazi kwa hiyo mashabiki wake mkae tayari kupokea ngoma yake mpya kwani soon anatarajia kuachia ngoma hiyo aliyowashirikisha member wa kundi ilo.
Baby Madaha kwa sasa unaisikia sauti yake kwenye ngoma ya Juma Nature kwa jina la “Narudi Kijijini” iliyotengenezwa Bongo Records ukiwa ni ujio mpya wa Nature.
SOURCE : deejay jona

No comments: