Thursday, November 8, 2012

OMMY DIMPOZ APATA SHAVU MAREKANI NA CANADA

 
Ommy Dimpoz baada ya kufanya vizuri na ngoma zake mbili “Nai Nai” na “Baadae” kupelekea kupata mafanikio mengi kupitia muziki wake.Msanii huyu ameanza kuona matunda ya muziki wake baada ya kupata shavu la kufanya Tour chini Marekani na Canada.
Mkurugenzi mtendaji wa wa Kampuni ya DMK GLOBAL PROMOTION & NORTHERN ZONE ENTERTAINMENT yenye matawi yake USA, UK na Tzee, Mr Dickson Mkama alias “DMK” amethibitisha habari zilizokuwa zinavuma hivi karibuni kuhusu kusaini mkataba na msanii Ommy Dimpoz kwa ajili ya Tour za kimziki ndani ya nchini ya Marekani na Canada.
Latest infoz kutoka kwa DMK ni kuwa watashirikiana na “J & P ENT” kuwaletea ziara ya ya mwanamuziki huyu, huku tarehe na Miji itatangazwa hivi karibuni pindi taratibu zote zitakapokamilika. Meneja wa Ommy Dimpoz kwa jina la Mr Mubenga pia amethibitisha habari hizi pamoja na picha wakiasaini mkataba.
Ukuachilia mbali Dimpoz, Mr DMK amesema ziara za wanamuziki kama Barnaba, Shetta na Linah zitafuta huko USA na Canada hivyio mkae tayari. Kwa maelezo zaidi piga simu number hizi USA +1 301-661-6207 au TZ +255784715993.
Source :deejay jona

No comments: