Sociedad wamemuajiri Moyes wakimpa mkataba wa miezi kumi na nane ambayo ni sawa na mwaka mmoja na nusu ambapo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jagoba Arrasate ambaye alifukuzwa kazi kufuatia timu hiyo kupata matokeo mabaya katika michezo yake ya ligi .
David Moyes ambaye amekuwa nje ya mchezo wa soka bila ajira yoyote kwa miezi 10 tangu alipofukuzwa kazi na Manchester United alichukua takribani wiki moja kabla ya kufikia uamuzi wa kuichukua klabu hiyo japo alishindwa katika jaribio lake la kumshawishi beki wa zamani wa Manchester United Phil Neville kuungana naye kama msaidizi wake .
Moyes ambaye ni raia wa Scotland anakuwa kocha wa tatu toka visiwa vya Ufalme Wa Uingereza yaani United Kingdom kuwa kocha wa klabu hii ya Real Sociedad waliopita kabla yake wakiwa John Tosha na Chirs Coleman wote wakitokea Wales .
No comments:
Post a Comment