Friday, November 14, 2014

Kifo cha Geez Mabovu chamfanya Dark Master kutangaza kuokoka

Baada ya kifo cha msanii wa miondoko ya Hip hop hapa nchini Tanzania aliyekua akiiwakilisha Iringa Geez Mabovu  rapper tokea Chemba squad na East zuu Dark Master amesema kuanzia sasa anaokoka.

 kwa kuacha kufanya maovu na kuacha kunywa pombe na kuvuta sigara, Ameyasema hayo jana kupitia show ya Street Bamiza ambayo inaandaliwa na Mtangazaji Nelly Be kupitia Nuru fm 95.3 redio iliyopo mkoani Iringa wakati wakizungumzia kuhusiana na kifo cha msanii Geez mabovu ambaye alikua mwanakundi au mwanafamilia wa Chemba squard na East zuu.
Sauti ya interview aliyofanyiwa dark Master kupitia Redio Nuru fm nitakuwekea kupitia mfululizo wa post zetu zijazo.

No comments: