Monday, November 17, 2014

Said Fellah Afurahia Yamoto Band Kubadili Upepo wa Muziki Nchini

Kiongozi wa familia kubwa ya muziki nchini mkubwa na wanawe Saidi fellah anasema anafurahia kuona mabadiliko makubwa ya kimuziki ambayo kundi lake la Yamoto Band yamelipata pamoja na ukweli kua limebadili upepo kwa baadhi ya wasanii wa bongofleva walioamua kufanya muziki wa bendi.
Fellah Afurahia Yamoto Band Kubadili Upepo wa Muziki Nchini
Akizungumza na tovuti ya Times fm fellah amesema kua anafurahi kuona kua kundi la Yamoto Band limerudisha ladha na ushindani wa muziki wa band nchini na kusema kua inampa moyo kuona kitu alichokisimamia kikikleya faida kwa jamii ya wanazmuziki


“Kama tumefanya kitu na watu wengi wamekipokea na wengine wakaona kama itawapatia nusura kwa kupitia idea hyo nawakaribisha tushindane “ amesema Fellah

fellah amesema pia kua wanaendelea kujiandaa kutoa nyimbo nyingi na nzuri zaidi li kudhihirisha ni kwa jinisi walijipanga

Yamot Band wanatarajia kuachia nyimbo mpya mapema mwaka ujao

No comments: