Nafasi tano za watangazaji wanaozitengenezea media zao mkwanja wa kutosha na kufanya redio kujulikana zaidi na kuwasogeza wasikilizaji wengi zaidi na kumshawishi mdau kuweza kutangaza na redio husika.
Utaratibu huu utakua ni kwa kila j5 ya kila wiki na hii idea
ni ya kwanza kabisa katika ulimwengu wa blog hapa Tanzania sio mbaya kama
ukiona inafaa na kuindeleza kwenye chanzo chako Team Djjonamusic blog na Radio
imekaa chini na kuona bora kuanzisha hizi chati.

Nafasi ya tano imekamatwa na Dokta joe huyu jamaa ni
mtangazaji wa kituo cha redio cha Ebony fm iliyopo mkoani Iringa, jamaa
anaendesha show inaitwa The splash hii show huluka kuanzia jumatatu mpaka
ijumaa time ni saa saba na robo mpaka kumi kamili.

Nafasi ya nne imeshikiliwa na Fadhili haule ambaye ni
mtangazaji wa redio Times fm iliyopo
hapa Dar na show ambayo anaiendesha inaitwa Sunrise ni kila siku za wiki
namaanisha j3 mpaka ijumaa.

Nafasi ya tatu imeshikiliwa na Renatus Bizzo kiluvia ambaye
ni mtangazaji wa Redio free Africa iliyopo jijini mwanza show inaitwa Showtime
New chapter ni kila siku za wiki.

Nafasi ya pili imeshikiliwa na Julias Kamafa uyu jamaa ni mtangaza
wa redio 5 iliyopo njiro Arusha show anayoiendesha inaitwa Funiko Baze ni kila
siku za wiki j3 mpaka ijumaa.

Na kwa hii wiki nafasi ya kwanza imeshikiliwa na B12 aka The
navigator wote mnafaham uyu jamaa yupo pale Clouds fm show inaitwa XXL time saa
saba kamaili mpaka kikumi kamili.
No comments:
Post a Comment