Member wa kundi la miaka ya 90 Fugees, Wyclef Jean anatarajiwa kuwa nchini Kenya weekend hii, ambapo atatumbuiza kwenye jukwaa moja na wasanii wengine wa Africa akiwemo Shaa kutoka Tanzania, katika fainali za msimu wa pili wa Coke Studio Africa.
Wasanii wengine wa Afrika watakaotumbuiza kwenye fainali hizo ni pamoja na Chidinma wa Nigeria, Navio wa Uganda, Rabbit wa Kenya na Neyma wa Msumbiji.
No comments:
Post a Comment