Blatter Adaiwa “kuchepuka” na ‘ex’ wa Cristiano Ronaldo.
Rais wa FIFA aliyetia aibu Sepp Blatter
ametajwa kuwa mpenzi wa zamani wa mwanamitindo Irina Shayk ikiwa ni kisa
kinachotikisa vichwa habari duniani kote. Gazeti la kila siku la
Hispania la El Mundo limechapisha madai hayo kuhusu mkuu huyo wa soka
mwenye macho makali na mpenzi wa zamani wa Cristiano Ronaldo katika
habari iliyochapishwa jana ikiwa na kichwa “Wanawake wote katika maisha
ya
Sepp Blatter.” Ilitangazwa kuwa babu huyo, 79, alikuwa na uhusiano na
mrembo huyo wa Urusi baada ya kuwa na mahusiano na mcheza tennis Ilona
Boguska lakini kabla hajakutana na mlimbwende Linda Barras, 50. Blatter
alianza kumuona mzaliwa wa Poland Ilona, rafiki wa binti yake Corinne,
mwana 1995 ambapo waliachana mwaka 2002, inavyodaiwa. Walirudiana tena
baada ya ndoa fupi ya Blatter mwaka 2002 na Graziella Bianca – mkufunzi
wa pomboo ambaye pia alikuwa rafiki wa binti wake.
No comments:
Post a Comment