SHOCKING!! Kumbe JOKATE Ashawai Taka Kujitia Kitanzi.
Sexy lady Mtafutaji Anayejishughulisha na fani lukuki ikiwemo urembo na
muziki, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ kwa mara ya kwanza ameweka wazi kwamba
alitaka kunywa sumu kisa kikiwa ni kuumizwa kimapenzi na mwanaume
aliyempenda kupindukia, aya zifuatazo zimesheheni. Akizungumza na gazeti
la 'Ijumaa Wikienda' , wikendi iliyopita, Jokate au ukipenda Jojo
alifunguka kwamba, japokuwa haikujulikana kwa watu wa nje kutokana na
usiri mkubwa uliofanywa na ndugu zake, akiwemo mama mzazi, lakini ameona
ni vyema akaweka wazi ili watu wajifunze namna ambavyo mapenzi yanaweza
kuharibu mustakabali mzima wa maisha ya mtu. Jokate ambaye amewahi
kutajwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mastaa mbalimbali Bongo

wakiwemo staa wa mpira wa kikapu ambaye ni Mbongo anayekipiga nchini
Marekani, Hasheem Thabeet Manka, wanamuziki, Ali Saleh Kiba na Nasibu
Abdul ‘Diamond Platnumz’ alisema hakuona sababu ya kuendelea kuishi bila
mwanaume huyo na kuona njia pekee ni kujitoa uhai. Jokate alikiri
kujifungia ndani Mara kwa mara na kujaribu kunywa sumu lakini alikuwa
akishtukiwa na ndugu zake hivyo kushindwa kutekeleza zoezi hilo.
Alisema kufuatia hali hiyo, ilibidi awe chini ya uangalizi maalum, huku
akiwa anaishi kama mfungwa na mara nyingi akipewa ushauri wa
kisaikolojia na baadaye kujikuta akimfuta mwanaume huyo moyoni. “Wewe
acha tu, hakuna kitu kinachouma kama mapenzi, niliumia mno, ilikuwa
mbaya mno kwangu kwani nilitaka kujiua baada ya kuona kabisa siwezi
kuishi bila huyo mwanaume kwa sababu nilimpenda sana tena sana.
Nilijaribu kunywa sumu mara kadhaa lakini nilikuwa naokolewa na ndugu
zangu, nashukuru nilipewa uangalizi maalum kutoka kwa ndugu,Unajua
ukiniona huwezi kujua kama huwa naumizwa na mapenzi kwa sababu mimi ni
msiri sana kwa mambo yangu binafsi kama hayo,” alisema Jokate akionekana
ni mtu ambaye akipenda huwa anapenda.
No comments:
Post a Comment