Sunday, June 28, 2015

Faiza: Najuta kuvaa nguo iliyoniacha maungo wazi >>>>>>>

Mwanadada Faiza Ally, amekiri kujutia uamuzi wake wa kuvaa nguo ya nusu utupu na kuacha maungo yake wazi kwenye Tuzo za Kilimanjaro akiwa na nia ya kuwa tofauti na watu wengine jambo lililopelekea kupokonywa mtoto wake na mzazi mwenzake ambaye ni Mbunge Joseph Mbilinyi. Amedai kuwa kamwe hawezi kurudia kosa na kusema kuwa atakuwa makini sana katika mavazi yake na kusema kuwa alibuni vazi lile akiwa na nia ya kuonekana tofauti lakini alijikuta akiumbuka baada ya kuwa kivutio kwa mashabiki.  Faiza: Najuta kuvaa nguo iliyoniacha maungo wazi >>>>>>> Mwanadada Faiza Ally, amekiri kujutia uamuzi wake wa kuvaa nguo ya nusu utupu na kuacha maungo yake wazi kwenye Tuzo za Kilimanjaro akiwa na nia ya kuwa tofauti na watu wengine jambo lililopelekea kupokonywa mtoto wake na mzazi mwenzake ambaye ni Mbunge Joseph Mbilinyi. Amedai kuwa kamwe hawezi kurudia kosa na kusema kuwa atakuwa makini sana katika mavazi yake na kusema kuwa alibuni vazi lile akiwa na nia ya kuonekana tofauti lakini alijikuta akiumbuka baada ya kuwa kivutio kwa mashabiki. Amesema kuwa naomba msamaha na kuendelea kuomba msamaha kwa jamii nzima kwani amejikuta katika wakati mgumu sana kwani hakuna mtu ambaye alimshtukia kuwa maungo yake yako wazi hadi anapigwa picha na mapaparazi katika zulia jekundu. Amesema kuwa ni kweli amezoea kuvaa nguo fupi lakini watu wasichukue tukio hilo kuendelea kusambaza picha hizo kwani kuna leo na kesho na kudai kuwa binadamu wanafanya makosa kwa nyakati tofauti. Ameongeza kuwa katika hali aliyonayo kwa sasa huenda mtu mwingine angekuwa mlevi au kufanya chochote lakini anamshukuru Mungu ana maamuzi ya kubadilika na kukiri kumpenda sana mtoto wake na hataki kuwa mbali naye.  By @sameerbryAmesema kuwa naomba msamaha na kuendelea kuomba msamaha kwa jamii nzima kwani amejikuta katika wakati mgumu sana kwani hakuna mtu ambaye alimshtukia kuwa maungo yake yako wazi hadi anapigwa picha na mapaparazi katika zulia jekundu. Amesema kuwa ni kweli amezoea kuvaa nguo fupi lakini watu wasichukue tukio hilo kuendelea kusambaza picha hizo kwani kuna leo na kesho na kudai kuwa binadamu wanafanya makosa kwa nyakati tofauti. Ameongeza kuwa katika hali aliyonayo kwa sasa huenda mtu mwingine angekuwa mlevi au kufanya chochote lakini anamshukuru Mungu ana maamuzi ya kubadilika na kukiri kumpenda sana mtoto wake na hataki kuwa mbali naye.

No comments: