FAIZA: WATANZANIA NISAMEHENI JAMANI >>>>>
Mzazi Mwenzake na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph
Mbilinyi ‘Sugu’ Faiza Ally, hivi karibuni katika tuzo za KTMA aliwaacha
watu midomo wazi baada ya kutinga na kivazi kilichoacha sehemu kubwa ya
makalio yake nje na kuzua minong’ono katika mitandao ya kijamii.
Akizungumza na Amani kwa kuonekana kujutia
kitendo kilichotokea, Faiza
alisema kuwa ile nguo aliishona ikiwa imeziba sehemu yote ya nyuma
japokuwa ilikuwa imechanwachanwa lakini hakuwa na nia ya kuacha sehemu
ya makalio yake nje.Akiendelea kuzungumza alisema kuwa, siku alipokuwa
akienda kwenye tuzo alikuwa peke yake kwenye gari hivyo alivyoinuka
ndiyo ile nguo ikapanda bila kufahamu.“Jamani siwezi hata siku moja
kujiachia hivyo naomba Watanzania wanisamehe,” alisema.
No comments:
Post a Comment