Wednesday, June 17, 2015

Mr. Blue ‘akiri’ mke wake kumpiga stop uvutaji Bangi >>>>>>>>

Mwanamuziki Wa Bongo Flava Mr.Blue ametoa ya moyoni kuwa mke wake ndiye aliyemfanya aache vilevi vyote ikiwemo bangi, fegi, mirungi pamoja na pombe. Kupitia ukurasa wake wa Istagram amesema “Alhamdulilahi ..nimeamka salama nikiwa mwenye furaha ahsante mungu ..na nashukuru pia kwa kufaulu  mtihani ahsante mke wangu @wahyda_bysers_heart kwa kunifanikisha kuacha vilevi vyote..(bangi, fegi, mirungi, pombe) na kuishi km binadamu wa kawaida..nawashauri ndugu zangu kuwa makini na marafiki wengine wapo kwa ajili ya kukuharibia maisha yako ..kuwa makini” Wanao tumia vilevi hivyo wanancho cha kujifunza hapo,chukua hatua kabla haujaharibikiwa.

No comments: