Mwana FA: Sifanyi collabo za nje sababu sioni kama zina faida yoyote kwenye muziki wangu
Sio ngumu kwa Mwana FA kupata collabo za
wasanii wa nje ya Tanzania kama akiamua, kwasababu rafiki yake wa karibu
AY ana connection na wasanii wengi wa Afrika na nje ya Afrika. Lakini
Binamu hana mpango huo kwasasabu haoni kama zina faida yoyote kwenye
muziki wake. “Nafikiri nawafanyia muziki watu wangu wa hapa,” Mwana FA
ameiambia 255 ya Clouds Fm. “Na ilivyo ni kwamba ukiangalia mi
naandika
zaidi AY anafanya ma-fleva zaidi, kwahiyo anaweza kufanya muziki ambao
lugha mtu haielewi lakini aka bang nao. Mi nafanya conscious ile hata
kila mtu anayeniskiliza aelewe nini nachosema, na lugha ninayotumia
inafanya watu wanaoweza kuskiliza muziki wangu ukawashika moja kwa moja
ni watu wanoongea Kiswahili kwahiyo sioni sababu ya kwanini
nijihangaishe.” Binamu ameongeza kuwa ikitokea kuna msanii wa nje
akahitaji kufanya naye collabo atakuwa tayari kufanya hivyo, lakini sio
yeye kutaka kufanya collabo na msanii wa nje. “Kama ntatoka kufanya
featuring nje ya nchi basi nataka nitoke kama msanii aliyehitajika
kutoka bongo sio kwasababu mimi nataka kufanya tu sioni kama inafaida
kwenye muziki wangu.” alimaliza.
No comments:
Post a Comment