Wastara ‘awachana’ wanasiasa >>>>>>>
Msanii wa filamu
nchini Tanzania, Wastara Juma, amedai kuwa wanasiasa wanawatumia sana
wasanii katika kampeni zao na baada ya kufanikiwa wanawasahau na kuwaona
ni wasumbufu pale wanapohitaji msaada. Amesema kuwa kipindi wanasiasa
wakiwa wanauhitaji nao huwaona kama lulu na kuwatumiwa ipasavyo
lakini
mchakato ukiisha kuwaona kuwa hawafai, kitendo ambacho amedai sio kizuri
kwani wanatakiwa kukumbukwa wakati wote na sio katika shida tu. Amedai
kuwa kwa upande wake hapendi siasa wala hapendi kufungamana na mtu kwa
kuwa wasanii wanatumiwa sana muda huu kwa kuwa wanashida, na kudai kuwa
baada ya hapo wanawaacha solemba na wakihitaji msaada kusaidiwa jambo
lenye maslahi huenekana wasumbufu.
No comments:
Post a Comment