Wednesday, June 24, 2015

Mzee Majuto Amuunga Mkono Wema Sepetu >>>>>>

 Mzee Majuto kwa mara ya kwanza ameamua kufunguka kumuunga mkono Wema Sepetu kwa nia yake ya kutaka kuwa mbunge.Kupitia ukurasa wake mtandaoni, Mzee Majuto aliandika; Nisingependa kuyaongea
 
haya kwenye mfungu mtukufu ila kiundani ningependa kuonyesha umoja na kumuunga mkono wazo na lengo la Mwanangu kwa kuwa anaweza na amethubutu sasa isitokee wale wasiopenda maendeleo ya watu na taifa hili kuvuruga misingi na mipango madhubuti ya kuwapa nafasi vijana na hasa wanawake kushika hatamu na kuleta mabadiliko.Kapeleke mabadiliko Singida na Tanzania nzima. Muhimu ni kuwa na juhudi uwezo imani pamoja na uzalendo. Ujumbe huu pia ni kwa kila kijana na mwanamke mwenye lengo na nia ya udhubutu. Inshallah. Ramadhan Maqbul Waislam wote. Mzee Majuto alimaliza kwa kumtag Wema.

No comments: