
kuwekeza zaidi kwenye muziki wake.“Kitu kikubwa nashukuru Mungu kwamba kazi ninayoifanya muziki na kile nilichokisoma vinakuwa vinakutana yaani vinashabihiana, kwasababu nimesomea Public Relations and Marketing, Public Relation ndio ni kudeal na mahusiano na watu mbali na hapo Marketing ndio biashara yenyewe kwa hiyo ina maana muziki wangu nitaufanya zaidi kisomi pasipo kukurupuka, kwa hiyo nita-invest zaidi katika muziki wangu kama biashara kubwa.”Ameongeza kuwa hana mpango wowote wa kuajiriwa kwa sasa, na hata ikitokea fursa labda itakuwa kwa baadae.“Mimi moyo wangu ulishakataa kuja kuajiriwa lakini itakapotokea kazi imetokea labda baadae, lakini sasa hivi nitakuwa na biashara zingine tofauti lakini kazi kubwa ambayo itakayokuwa inaniingizia kipato kwenye biashara zingine ni muziki.”
No comments:
Post a Comment