
Mwanamuziki Wa muziki wa Hip Hop nchini Tanzania, Emmanuel Elibariki ukipenda ‘Nay Wa Mitego’ ameamua kuwekeza kwa watoto wake kwa kuwawekea mazingira bora ya kupata elimu ikiwemo kuwanunulia gari la kuwapeleka shule. NAY Amesema kuwa hataki watoto wake Curtis na Munie, wasome kwa shida kama yeye alivyosoma kwa taabu, na ndiyo maana amewanunulia gari la kuwapeleka shule. Amedai kuwa gari hilo lina vitu muhimu ndani kama meza ya kulia chakula, sinki la kunawia mikono, kitanda cha kulalia,TV na huduma nyingine ambalo wataanza kulitumia mwakani na kusema sasa anatafuta dereva atakayekuwa akiwapeleka shuleni.
No comments:
Post a Comment