Tuesday, July 7, 2015

'Tuzo za KTMA Zilikuwa Haki Yangu' Asema ALIKIBA >>>>>>>

 Mwanamuziki nchini Tanzania, Ali Kiba, ambaye amejitokeza tena katika ulingo wa muziki baada ya kupumzika kwa miaka mitatu amepuuzilia mbali madai kwamba alipendelewa katika tamasha la tuzo za Kilimanjaro. Ali kiba, ambaye alipata tuzo sita amesema kamwe hakupendelewa na kwamba ni muziki wake
 unaopendwa na wengi tofauti na baadhi ya watu wanavyofikiria. Akihojiwa na runinga ya Citizen wikendi iliyopita alisema kuwa anahisi yeye ndio bora na kwamba ilikuwa haki yake kushinda tuzo hizo kutokana na kujituma ili kuweza kuwapa mashabiki ladha iliyopotea kwa muda na ndio maana alitwaa tuzo sita kati ya saba alizoteuliwa. Sambamba na hilo amedai kuwa hana beef na mwanamuziki mwenzake Diamond, na kusema kuwa anakerwa sana watu wakilinganisha na msanii huyo na kudai kuwa yeye ni yeye na Diamond ni Diamond.

No comments: