Joh Makini amesema kuwa mipango ya
collabo kati yake na staa wa Nigeria, Davido ilianza muda mrefu lakini
hakutegemea kama mwimbaji huyo wa ‘Aye’ angechukua uamuzi wa kuiweka
hadharani kipindi hiki. Weekend iliyopita (Sept 18) mashabiki wa muziki
Tanzania walipokea kwa furaha habari njema kuhusu ujio wa collabo ya
East na West kutoka kwa Davido mwenyewe ambaye alitweet: DAVIDO X JOH
MAKINI COMING SOON — Davido September 18, 2015. Joh ameiambia Djjonamusic kuwa Davido alianza kuvutiwa

na kazi zake alipomshuhudia kwenye jukwaa la Fiesta, ambapo Davido pia
alikuwa miongoni mwa mastaa wa Kimataifa waliotumbuiza kwenye tamasha
hilo jijini Dar es salaam. “Hii kusema kweli imeanza kitambo na mchizi
alikuwa ananifatilia, nakumbuka mara ya mwisho kuna show moja ilifanyika
kubwa Leaders (Fiesta) na mchizi alikuwepo, sasa wakati wa performance
yangu na jamaa alikuwepo, sasa kuanzia pale jamaa alikuwa ananiulizia
who is this guy watu wakawa wananiambia, yaani alikuwa surprised show
ilikuwa kubwa…” Ameongeza kuwa baada ya kupata feedback kutoka kwa watu
mbalimbali kuwa Davido anamzungumzia vizuri na anatamani kufanya naye
kazi aliamua kutumia fursa hiyo kuwasiliana naye kwaajili ya kufanya
kazi. “Sasa vitu kama hivi vinapokuja inabidi na wewe ujiongeze kidogo,
tukamcheki kama kuna uwezekano wa kufanya kazi na mchizi, na mchizi
mwenyewe akasema alikuwa anataka sana kufanya kazi na mimi” Joh amesema
kuwa tayari wameanza maandalizi ya kufanya wimbo huo licha ya Davido
kuweka wazi mapema bila yeye kutarajia. “Sema yeye nafikiri amekuwa na
haraka sana kuipeleka kwenye media lakini sio mbaya.” alisema Joh. Bado
haijajulikana wimbo watakaofanya utakuwa ni wa nani, lakini Joh amesema
inaweza ukawa wa wote wawili, lakini kazi ikishafanyika watafanya
mazungumzo kuamua juu ya hilo. Hii itakuwa ni collabo ya tatu ya
kimataifa kwa Joh Makini kwa mwaka huu, baada ya ile ya AKA pamojan nay a
K.O ambayo nayo bado iko kwenye maandalizi.
No comments:
Post a Comment