Ikiwa ni miezi 5 tu imepita toka Benard “Ben Pol” Paul atangaze kusaini
mkataba wa usimamizi na kampuni ya Panamusiq, mwimbaji huyo wa R&B
amevunja nao mkataba.Bongo5 imemtafuta Ben Pol ili kuzungumzia sababu za
kusitisha mkataba huo ambao wakati wanasaini walisema ungekuwa ni wa
muda mrefu (Ingia hapa ). “Unajua tumeanza kufanya kazi mwezi wa 4 na
tumeachana mwezi wa 9” alithibitisha kusitisha

mkataba. Ben Pol amesema
kuwa kwa kipindi cha miezi 5 ambacho amekuwa na kampuni hiyo kuanzia
mwezi April hadi September 2015 alipousitisha mkataba, amekuwa akiweka
rekodi ya utendaji na kwa namna fulani kuna vitu ambavyo hakuridhishwa
navyo japo hakutaka kuweka wazi sababu halisi ya kusitisha mkataba.
Ameongeza kuwa alikaa mezani na kampuni hiyo na pande zote mbili
wakakubaliana kusitisha kufanya kazi, na kuwa wameachana kwa uzuri. Pia
amesema wamekubaliana kutotoa tamko rasmi wala kuzitaja sababu za
kuachana. Alhamisi ya wiki hii (Sept 24) Ben Pol ataachia single mpya
‘Ningefanyaje’ aliomshirikisha Avril wa Kenya.
No comments:
Post a Comment