Mwimbaji wa muziki wa
mduara AT amesema wakati yupo chini ya management alikuwa haoni faida ya
muziki wake. Akizungumza na Story Tatu ndani ya kipindi cha Planet
Bongo cha EA Radio, AT amesema Tanzania hakuna mameneja wa muziki bali
kuna madalali. “Tanzania hakuna management kuna madalali tu,”

alisema.
“Wakati nasimamiwa nilikuwa sioni faida ya muziki ninaofanya lakini
baada ya kuanza kujisimamia mimi mwenyewe kama mimi, nilipata kuelewa
kwanza muziki ukoje na una ugumu gani, na kipato chake ni kipi,”
alisisitiza. “Meneja maana yake ni mfanyakazi wa msanii, lakini Tanzania
meneja ni bosi analala anategemea msanii apate show yeye ndo ale. Yeye
hawezi kutafuta show, meneja hawezi akamkodia msanii nyumba, gari,
akamtengeneza msanii sera za kule anakokwenda. Anachosubiri ni show,
akishakuona unaanza kulegalega uwezo umepungua anakuacha.”
No comments:
Post a Comment