Izzo Business ameweka wazi kuwa kwa nafasi yake, anasaidia kunyanyua
vipaji vya wasanii wanaochipukia kwa kutenga muda wake kutoa ushauri
kama ambavyo binafsi ameweza kufanikiwa kwa kuzingatia mawazo na
kujifunza kutoka kwa wasanii waliomtangulia
Akiongea na East Africa Radio, Izzo alijitolea mfano yeye mwenye , Alisema
“Mimi mara nyingi sijafikia uwezo wa kuwachukua watu kuwasaidia kuwapeleka
studio, kuwalipia video na nini, lakini kwa mtu ambaye naona ana nia na
malengo kwasababu hata mimi nilifight, walikuwepo kina Sugu kina nani
ambao walikuwepo juu yangu, wakina adili, kikubwa ambacho nilikua
nachukua kwao ni mawazo na kuangalia ambacho walikua wanafanya”
Pia Izzo ameeleza kwa wasanii wenye malengo ya kukua na vipaji ndani
yao, huwa anachukua nafasi ya kuwajenga wawe wasanii bora wa baadaye,
ushauri wake wa wazi kwao pembeni ya muziki ukiwa ni displine, heshima
kwa kila mtu na kuzingatia muda.
No comments:
Post a Comment