Pamoja na changamoto kadhaa, mwaka 2015 umekuwa
na mafanikio kwa Barnaba ikiwa pamoja na kufanikisha kurekodi wimbo na
msanii wa Uganda, Jose Chameleone. Barnaba amesema mwaka huu amefanikiwa
kujenga msingi nzuri wa muziki wake kwenda kimataifa ambao utampa
mafanikio mwakani. “Huu ni mwaka mzuri, nimefanya vizuri kwa kiasi
chake, pia mafanikio yangu makubwa yapo kwenye

kutengeneza connection za
kwenda kimataifa zaidi,” ameiambia Bongo5.“Nina matumaini mwaka 2016
Barnaba atakuwa Barnaba mpya kwenye tasnia yetu ya muziki na kuwapa
matumaini mapya mashabiki wangu ambao walikuwa wakiumia,” ameongeza.
“Kuna video kubwa inakuja na Chameleone sitaki kusema nitafanyia wapi
lakini ni kubwa. Pia kuna kolabo nyingine kubwa na msanii wa Uganda,
kwahiyo nafunga mwaka kimataifa zaidi.”
No comments:
Post a Comment