Monday, November 16, 2015

Nick Minaj kupewa tuzo ya heshima ya ‘VH1 Big in 2015′

Nick Minaj ataongeza idadi ya tuzo kwenye kabati lake siku ya sherehe za “VH1 Big in 2015 with Entertainment Weekly” ambapo atapewa tuzo ya heshima.
Nicki Minaj
Tuzo hizo za heshima utolewa kila mwaka kwa watu ambao wametoa burudani zaidi kwa mwaka huo, Nick Minaj ataungana na wasanii wengine ambao tayari wametangazwa ikiwa ni pamoja na  Taraji P. Henson, Amy Schumer, Aziz Ansari na O’Shea Jackson, Jr. ambaye anapewa tuzo hiyo kwa niaba ya waigizaji wote wa filamu ya  ‘Straight Outta Compton.’
Sherehe hizo zitakuwa hosted na rapper T.I tarehe 15 Nov. kwenye ukumbi wa the Pacific Design Center,Los Angeles na zitaoneshwa rasmi tarehe 7 Dec kwenye kituo cha VH1.

No comments: