Msanii ambaye yupo chini ya Label ya Diamond Platnumz ‘WCB’, Harmonize amesema wimbo wa msanii mkongwe wa Bongo Fleva Q chillah ‘For you’ umetokana na wimbo wake wa ‘Kidonda changu’
Akiongea na AyoTv, Harmonize amefunguka kuwa Q chillah aliwahi kumuomba aimbe wimbo wake huo wa ‘Kidonda changu’ baada ya kuusikia kwa Mazuu kabla hajatoka kimuziki lakini alimshauri waandike wimbo mwingine kwasababu yeye mwenyewe alikua ameweka matumaini makubwa kupitia wimbo huo “Nikamwambia sasa Bro embu tufanye kitu kimoja, kwani ulichopenda kwenye huu wimbo nini, akanambia kidogo nimependa
maneno yake lakini pia Beat ni miendo ya kisasa ambayo inafanya vizuri” ameelezea Harmonize
“Nikamwambia sasa bro sikiliza embu tufanye kitu kimoja, ngoja tuvue haya maneno alafu tucreate vitu vipya kwasababu tukiwa tunacreate maneno mapya me naamini hata mwenyewe utakua na maneno yakuongezea pia, nyimbo itakua nzuri zaidi kuliko ukiimba kama nilivyoimba mimi” Harmonize ameongeza kuwa hapo ndio akatengeneza wimbo wa For You
Usikilize ‘Kidonda changu’ wa Harmonize hapo chini
No comments:
Post a Comment