Wednesday, November 11, 2015

Belle 9 asema aliwahi kushinda Tuzo Ujerumani, kuwaonesha mashabiki wake kwenye Project Ijayo

Muimbaji wa ‘Shauri zao’ Belle 9 amesema mbali ya kuwa hajawahi kushinda Tuzo yoyote ya ndani ya nchi lakini kitu ambacho watu wengi hawajuhi ni kuwa amewahi kupewa Tuzo nchini Ujerumani.

IMG-20140826-WA0001
 Belle 9 amesema Tuzo hiyo alipewa jijini Berlin nchini Ujerumani na mashabiki wake watapata nafasi ya kuiona kwa mara ya kwanza kwenye video yake itakayofata baada ya ‘Shauri zao’
“Ofcourse nimeshawahi kufanya show nyingi nje ya Tanzania, na pia nje ya show nimeshawahi kupewa hata award, nimeshawahi kupata award German,Berlin pale nakumbuka nishapewa award kabisa ambayo hiyo award watu wataiona kwa mara ya kwanza kwenye video yangu mpya ambayo itatoka …” Alisema Belle 9

No comments: