Wimbo mpya wa Barnaba Classic aliomshirikisha staa wa Uganda, Jose Chameleone ndio collabo ya kwanza ya kimataifa kwa Barnaba. Barnaba ambaye anauachia wimbo huo ‘Nakutunza’ leo November 9, amesema kuwa video ya wimbo huo itachelewa kutokana na kwamba yeye binafsi anauogopa wimbo huo, akimaanisha ni wimbo mkubwa hivyo anaogopa
kukosea. “Video yangu imechelewa kwasababu wimbo huu ndio collabo yangu ya kwanza inayonipeleka International na ndio collabo yangu kubwa” alisema Barnaba kupitia 255 ya XXL. “Video yake itachelewa zaidi kutokana na kwamba ni wimbo wangu ambao nauogopa.”
Barnaba ameweka wazi kuwa mpango uliopo ni kufanya video kubwa nje ya Tanzania. “Hii collabo ya Jose ni kubwa kidogo na nimeifanya kwenye umahiri mkubwa kwa kiasi kwamba huu wimbo nauogopa…Of course nawaza nifanye nje ya Tanzania lakini nawaza ni wapi na nifanye kwa namna gani , nimewapa baadhi ya watu wanaondika script vizuri waandike kwasababu nataka nifanye video ya kunipeleka international “ alimaliza Barbana.
No comments:
Post a Comment