Exclusive:Sababu za Q Chief kujiondoa kwenye kampuni ya QS J MHONDA,MHONDA aelezea sababu
Staa
wa muziki nchini, Abubakar Katwila aka Q Chief amevunja mkataba wake na
label ya muziki ‘QS J Mhonda’ kwa madai kuna vitu ambavyo haviendi
sawa. Chief ameiambia Bongo5 kuwa ameamua kujitoa rasmi katika label
hiyo ili asimame mwenyewe. “Mimi bhana naomba uwaambie mashabiki wangu
pamoja na watanzania, sipo tena na QS J Mhonda,” amesema Q Chief.
“Nimeamua kujitoa kwa sababu kuna vitu haviendi sana, sasa siwezi
kuendelea kukaa bora nijitoe.” Kutokana na hatua hiyo Djjonamusic Blog ilimtafuta
Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Mhonda aliyeeleza kwa upande wake
kilichotokea.
“Kilichomuumiza Q Chief ni kuona mimi nawasaidia wasanii wengine,” amesema.

“Mimi
kuwasaidia wasanii au watu mbalimbali ni sehemu ya maisha yangu sasa
yeye amekuwa akisema hadharani mbele ya wasanii wangu wadogo kwamba
hawapendi kuwaona wasanii wachanga anatamani hata kuwapiga bastola ili
asiwaone kabisa. Nimejitaidi sana kumweka sawa ili aendane na mimi au na
kampuni yangu lakini haonekani kubadilika na anaonesha roho mbaya kwa
wenzake tena ya wazi,” ameongeza.
“Hivi
karibuni niliamua kumuongeza Mzee Yusuf katika kampuni yangu yaani kuwa
miongoni mwa wasanii wangu na nikampeleka Afrika Kusini kwa ajili ya
video yake mpya, Q Chief akasirika kuona kwanini nafanya hivyo wakati
hata kwake namfanyia hivyo hivyo na kuzidi. Kwahiyo sasa mimi binafsi
hiyo taarifa imenishtua kwa sababu tayari nimeshatumia zaidi ya shilingi
milioni 60 mpaka sasa na bado anakaa kwenye nyumba yangu. Nikimpigia
simu ananiambia ‘ongea na mwanasheria wangu.’ Sasa mimi binafsi siwezi
kulizungumzia hili suala na ni hatua gani tutazichukua lakini naomba
ongea na mwanasheria wa kampuni yetu nadhani atakuwa na kauli.”
Djjonamusic Blog haikushia hapo, ilimtafuta mwanasheria wa kampuni hiyo, Joseph Mhina
aliyedai kuwa mkataba ndio utamhukumu msanii huyo kwani kila kipengele
kinaeleza hatua za kuchukuliwa endapo mteja atakiuka utaratibu.
No comments:
Post a Comment