Monday, January 11, 2016

Hii Ndio Sababu Ya ALI KIBA Kutofollow Mtu Kwenye Mtandao Wa Instagram

Ali Kiba ni star katika muziki wa bongo flava… kama wew ni mtumiaji wa Instagram, utakuwa umeona kuwa Ali Kiba hajafollow mtu yeyote, ukitembelea mitandao ya kijamii ya Ali Kiba utaona ya kuwa ana mashabiki wengi wanaomfuatilia kupitia mitandao hiyo.
 
Katika mahojiano na Djjonamusic Mkali huyo wa bongo flava alisema haya kuhusiana na swala la kutofollow mtu yeyote “Yea sifollow mtu kwa sababu kwanza kabisa nafanya kazi na watu wengi, kuna akina Dj jona kuna watu kibao lakini watu wa media ndio tuko nao karibu, sasa wengine walikuwa wakicomplain nikawa naogopa zile lawama nilichoshauriwa na hao wenyewe kwamba ni 

 heri nisifollow mtu na vile vile nilipenda hivyo kutokana na promotion ya ujio wangu ambao ulikuwa unakuja ili niweze kuconcentrate na account yangunijue mafans wangu wanataka kitu gani, wananiadvice kitu gani na pia imesaidia naona jinsi gani wako serious na mimi kwa sababu naongea nao, kuna wengine wanaipa challenge, kuna matusi uhmn ni vitu vya kawaida na vile vile wanapokuwa wananisema wananijenga kiasi fulani, wananibadilisha ni wapi nimekosea naweza kubadilisha”

No comments: