PICHA: 'Tazama Mjengo Wangu Huu Ukupe Hasira' - MADEE
Madee amesema aliamua kuonesha
mjengo wake baada kukamilika kwa madhumuni ya kuwatia hasira vijana
wenzake wanaochezea pesa. Madee ameiambia Djjonamusic kuwa licha ya kuonesha
picha

ya mjengo huo, bado ana nyumba nyingine iliyopo katika hatua za
mwisho. “Hii nyumba ipo Mbezi na tayari nimeshahamia,” alisema. “Hii ni
ya kwanza bado kuna moja naimalizia. Nawaonyesha makusudi ili kuwatia
hasira kwa sababu vijana wanachezea pesa bila kuwekeza au kujua kuna
kesho.” Katika hatua nyingine Madee amewataka mashabiki kusubiria kazi
nzuri kutoka kwake zitakazoanza kutoka hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment