Rappper mkongwe, Mr Blue amesema kuna sababu kubwa
tatu ambazo zilisababisha wasanii wa muziki wa kipindi cha nyuma
kushindwa kutoboa kimataifa. Blue ambaye anatamba na video ya wimbo
‘Baki na Mimi’, alikiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM Jumatano hii
kuwa moja ya sababu ni wasanii kuona wao ni wa hapa hapa.

“Ni kama vitu vitatu cha kwanza ninaweza kusema wakati tunaanza muziki soko letu tulikuwa tunawaza hapa na hizo nchi zetu za karibu ambazo ni Kenya na Uganda,” alisema.
“Kwahiyo kilichotufanya kutofika huko ni kutokujua hicho. Cha pili ni connection kwa sababu watu unaowaona wanachezwa kwenye hivyo vyombo vikubwa wengi sio kwamba wana video nzuri wengine ni connection na wale watu wa vituo,” aliongeza. “Na cha tatu ambacho kinasaidia kweli ambacho tulikuwa tunakidharau ni video kali. Kuwa na video kali nayo inasababisha hata watu wa kule pia kuipenda na kuoana kwamba kweli hii inafaa kuchezwa kwenye kituo chetu.
No comments:
Post a Comment