"Nikiongea Yaliyonitokea Na NUH ( Mtaumia Sana" Asema SHILOLE >>>>>>>
Shilole na Nuh Mziwanda wameuvunja rasmi
uchumba wao uliodumu kwa takriban miaka mitatu. “Mimi naye it’s over,”
Shilole ameiambia Djjonamusic. “Basi tu kuna vitu vingi vimetokea, siwezi tu
kuwa naye tena. Nitapenda tena lakini ntaangalia mtu ambaye tunaweza
kuendana, uelewa wa akili, uelewa wa kila kitu,”

ameongeza. Shishi
amesema alimvumilia sana Nuh lakini uvumilivu ulimshinda. “Ni kuamua tu,
vitu vinapozidi kuwa vingi halafu, unajua sisi wanawake Mungu ametupa
kitu fulani kwamba tuwatunze nyinyi wanaume na sisi huwa tuna upendo
sana, tuna uvumilivu wa vitu vingi sana lakini kuna wakati Mungu naye
anakuja kukupa moyo kwamba nadhani tu hapa pumzika, acha, ndicho
kilichonikuta mimi.” “Sababu yaliyonitokea ni makubwa, siwezi kuongea
kiukweli lakini nikiongea watu mtaumia sana. Siwezi kuongea ila mimi
moyo wangu umeridhika.” Shilole amesema kwa sasa yupo single and ready
to mingle!
No comments:
Post a Comment