Wednesday, January 13, 2016

Sina mpango wa kufuta Tattoo ya shilole lakini nimesikitika kwasababu amefuta yangu – Nuh Mziwanda

 Nuh Mziwanda amedai mbali ya kuachana na Shilole lakini hana mpango wa kufuta tattoo ya mrembo huyo.
Nuh amesema amesikitishwa na kitendo cha Shilole kufuta tattoo yake mara tu baada ya kuachana,
 
“Kiukweli nimesikitika sana hata kama tumeachana mimi mbona sijafuta tattoo zake na sina mpango wa kuzifuta kwa sasa”Alisema Nuh.

 SHISHI tattoo zamani
Hata hivyo Shilole alipoulizwa kuhusiana na alichokisema Nuh alisema kuwa mbona Nuh aliwahi kuwapost mademu zake wapya mara tu baada ya kuachana.
“Mimi nimewahi kufuta tattoo kwa sababu yeye alianza kuwapost mademu zake wapya Instagram baada ya kuachana” Alisema Shilole.

No comments: