Thursday, January 21, 2016

Wasanii Nyota Waongoza Kukwepa Mashirikisho Ya Sanaa >>>>>

Baraza la Sanaa la Taifa Nchini Tanzania (Basata), limeweka wazi kwamba wasanii wenye majina makubwa ndio wanaongoza kutokuwa wanachama wa mashirikisho ya wasanii.
Baraza hilo pia limeyataka mashirikisho na vyama vyote vya wasanii nchini kufanya uchaguzi ili 
 
kusaidia sekta ya sanaa iwe na mfumo bora wa utawala unaotambulika na kuheshimika na wadau, wasanii na Serikali kwa ujumla. Katibu mtendaji wa baraza hilo, Godfrey Mungereza, alieleza hayo jana alipokuwa katika mkutano wa majadiliano kati ya Baraza na wadau wa sanaa nchini. Baraza hilo pia limewataka wasanii wote nchini wajisajili ili wawe na vibali vya kazi za sanaa vitakavyowawezesha kushiriki kikamilifu kujenga mfumo wa utawala katika sanaa ambao utatumika kama mfumo sahihi na rasmi wa mawasiliano kati ya Serikali na wasanii.

No comments: