Saturday, February 20, 2016

Huyu Ndo Mpenzi Mpya Wa NUH MZIWANDA Baada Ya Kuachana Na SHILOLE

Msanii wa bongo fleva Nuh mziwanda baada ya kutemana na msanii mwenzake Shilole ameamua sasa hivi kuweka uhusiano wake mpya hadharani.

Kupitia akaunti yake ya instagram Iam_mziwanda Nuh amekuwa akimpost mara kwa mara mrembo anayetumia jina la _erah_erah_ kwenye mtandao huo. Kupitia mahojiano yake na Radio moja NUH alikiri kuwa huyo ndiye baby number one wake kwa sasa na anaishi Oman na amekuja Tanzania kwa muda tu. “Ni mpenzi wangu ila haishi hapa amekuja kutembea kwa sababu tulianza ku date tangu yupo nje kwa hiyo amekuja sa hivi tumeanza mapenzi yetu rasmi..yeye anaishi Oman” alifunguka Nuh na kusema kwa sasa hataki kuzungumza mengi anaangalia upepo kwanza.

No comments: