Thursday, February 18, 2016

Ray Aeleza Siri ya Weupe Wake

Baada ya kuandamwa na baadhi ya mashabiki wake katika mitandao ya kijamii kuhusu weupe wake, Ray Kigosi amesema kwamba yeye hajawahi kujichubua bali huwa anakunywa maji mengi pamoja na kufanya mazoezi.

Akizungumza katika kipindi cha ENewz cha East Africa Radio, Ray alisema kwamba huwa anakwenda saluni mara moja kwa wiki kwa ajili ya kusafisha uso wake (Scrub) ili akiwa anafanya kazi zake watu waweze kumwona vizuri na kupenda kazi zake. Muigizaji huyo aliyeachia filamu ya ‘Tajiri Mfupi’ hivi karibuni, alisema hajawai tumia mkorogo kama baadhi ya watu wanavyodai. Naye mpenzi wake Chuchu Hans amesema kwamba mpenzi wake hajichubui bali ni maisha yamemkubali tofauti na hapo nyuma alivyokuwa anahangaika kuinua sanaa na kipaji chake.

No comments: