Wednesday, March 16, 2016

DYNA :MUZIKI UMENIFANYA NIHESHIMIKE NA NIJITEGEMEE

Dyna Nyange Hit Maker wa #Nivutekwako na sasa #angejua amesema Mziki umemfanya kuheshimika katika jamii na kuondokana na utegemezi aliokuwa nao kwa ndugu. Akiongea na kipindi cha #Planetbongo cha #EARadio DYNA amesema amekuwa pia akijitahidi kuwa mfano mwema kwa jamii na Watu
 
 wanaomwangalia kama msanii na kama mwanamke pia. Dyna amesema mwanzo alikua akitegemea mahitaji muhimu kutoka kwa ndugu zake lakini siku hizi anaweza kujitegemea kwa 100% na yote hiyo ni kwasababu ya music. Kama mwanamke hiyo imempa heshima pia kwa jamii kuwa ameweza kusimama peke yake bila kumtegemea MTU.

No comments: