Friday, March 25, 2016

Nachukia Tunavyowashobokea Wanaijeria" – JUX

Jux amesema anaumia kuona jinsi Tanzania inavyowashobokea Wanaijeria na kutowapa heshima wanayostahili wasanii wa nyumbani.
Akiongea kwenye kipindi cha The Sporah Show, Jux amevishauri vyombo vya habari na wadau wengine wa muziki kujali uzalendo.

Ametolea mfano jinsi ambavyo redio zinavyoucheza muziki wa Nigeria kwa kiasi kikubwa kiasi cha kuwaaminisha wasikilizaji kuwa muziki wao ni bora zaidi.
“Mimi nachukia sana yaani, nikiona kuna msanii Bongo katoa nyimbo yupo halafu presenter anampigia simu msanii wa nje anatoa wimbo, wao kule hawatufanyii hivyo, wale hawatujali kabisa. Sio kwamba mashabiki hawatupendi, wanatupenda, sema hatujatengenezwa kama wanavyotengenezwa wale,” amesisitiza.
Amewaomba watangazaji na madj kuwasupport zaidi wasanii wa Tanzania.

No comments: