Friday, March 25, 2016

"Hip Hop Si Dini, Nimeamua Kuimba Kwa Kuwa Naweza Fanikiwa Kulingana Na Uwezo Wangu "-RAYMOND

Alifahamika kama mkali wa kuchana Ukipenda Freestyle za kutosha miaka ya nyuma na hakuna aliyefikiri angeweza kugeuka na kutengeneza hitsong kwa kuimba 100%. Wimbo Wake Mpya Inayokwenda Kwa Jina #kwetu Kaitambulisha juzi tu lakini impact yake ni kubwa kwasasa. RAYMOND ameweka wazi kuwa yeye alikuwa msanii wa Rap lakini hakuwa mwanaharakati wa hip hop kwasababu hip hop ukiifanya kama
 
 dini itakutesa. Raymond ameiambia #planetbongo kuwa wapo Watu ambao ni wanahip hop na hawafanyi rap kwahiyo Muziki wa hip hop siyo dini so ameamua kuimba kwa kuona anaweza kufanikiwa kulingana na uwezo wake na ushauri wa management yake (WCB) .
Hata hivyo ameweka wazi kuwa kipaji chake cha kurap bado kipo na ana nyimbo kibao alizorap zipo store na kila akipata mizuka ya kurap huwa anaandika mistari na kuitunza.

No comments: