Friday, March 25, 2016

PREZZO Awataka Wasanii Wapime HIV

Msanii Maarufu nchini humu , CMB Prezzo, amewataka wasanii wenzake nchini humo wakapime HIV kwa ajili ya kujua afya zao. Hilo limekuja baada ya kutambua majibu yake alipopima na kugundulika kwamba 
 
hana upungufu wa kinga mwilini. “Najua kupima HIV sio kazi ndogo, lakini ni kitu kizuri kwa maisha ya sasa hasa kwa vijana ambao tunajua nini tunakifanya. “Ni vizuri kwa wasanii kujitokeza kama mimi nilivyofanya, nashukuru Mungu majibu yangu mazuri, ila kilichobaki ni kujilinda,” aliandika Prezzo kwenye ukurasa wake wa Twitter.

No comments: