Meneja wa Tip Top
Connection, Babu Tale amesema msanii wake Madee tayari ana ngoma 6 mpya
ambazo hazitatoka, ambapo moja kati ya hizo ni kolabo yake na Tekno.
Akizungumza katika kipindi cha The Playlist cha Times FM, Babu Tale
amesema anasubiria wakati ufike aanze kuachia kazi hizo ambazo amedai ni
kali.
“Nina nyimbo sita mpya za Madee zinanichanganya,” alisema Tale.
“Kuna wimbo kafanya na Tekno, kuna ngoma tatu ameshafanya na video. Kuna
ngoma tunafanya video Jumatatu, nachanganyikiwa sijui nifanyeje kwa
sababu nina ngoma kali za Madee”, Aliongeza, “Wakati Madee anarudi kila
mmoja ataongea kama nambeba, lakini Madee kila mtu anajua ana mwaka
mmoja hajaachia ngoma”,
No comments:
Post a Comment